• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Iraq

  (GMT+08:00) 2019-09-23 20:36:56

  Rais Xi Jinping wa China hapa Beijing amekutana na waziri mkuu wa Iraq Bw. Adil Abd Al-Mahdi.

  Rais Xi amepongeza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Iraq, huku akisisitiza kuwa China inaunga mkono juhudi za Iraq katika kulinda mamlaka ya taifa, uhuru, umoja na ukamilifu wa ardhi, na kupinga nguvu yoyote ya nje kuingilia siasa za ndani ya Iraq. Amesema China inaipongeza Iraq kwa ushindi mkubwa katika mapambano dhidi ya ugaidi, na kupenda kuunga mkono na kuisaidia Iraq kufanya mapambano dhidi ya ugaidi na ujenzi mpya, na kutimiza usalama wa kudumu na maendeleo ya taifa.

  Bw. Al-Mahdi amepongeza maadhimisho ya miaka 70 tangu Jamhuri ya watu wa China kuanzishwa. Amesema China inalinda kithabiti mamlaka ya taifa, uhuru na heshima ya taifa na kupata maendeleo makubwa. Amesema China ni nguzo muhimu ya kulinda amani, utulivu na masikilizano ya dunia. Pia ameishukuru China kwa kutoa uungaji mkono muhimu kwa mapambano dhidi ya ugaidi na ujenzi mpya wa Iraq.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako