• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping atembelea Maonyesho ya mafanikio makubwa katika miaka 70 iliyopita tangu Jamhuri ya watu wa China kuasisiwa

  (GMT+08:00) 2019-09-24 08:57:48

  Rais Xi Jinping wa China ametembelea Jumba la maonyesho la Beijing na kuangalia Maonyesho ya mafanikio makubwa katika miaka 70 iliyopita toka Jamhuri ya watu wa China kuasisiwa.

  Rais Xi amesisitiza kuwa katika miaka 70 iliyopita, Chama cha Kikomunisti cha China kimewaongoza watu wa China kujipatia uhuru na kuwa na utajiri na nguvu zaidi. Matokeo makubwa yaliyopatikana katika miaka hiyo 70 yanaonyesha kuwa Chama cha Kikomunisti cha China ni chama pekee ndio kinachoweza kuiongoza China, ujamaa ni njia pekee inayoweza kuiokoa China, mageuzi na ufunguaji mlango ni sera pekee inayoweza kuiendeleza China, Usoshalisti na Nadharia ya Umarx, sera ya ujamaa wenye umaalum wa China ni njia pekee inayoweza kuistawisha China.

  Rais Xi anataka maonyesho hayo yaweze kuwahamasisha wananchi wote wajizatiti kufanikisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote, na kutimiza Ndoto ya China ya kurejesha ustawi wa taifa la China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako