• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TUZO: Lionel Messi amwangusha Cristiano Ronaldo kwenye tuzo za mwanasoka bora wa FIFA

  (GMT+08:00) 2019-09-24 09:42:57

  Straika wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa dunia katika Usiku wa Tuzo za FIFA Jijini Milan, nchini Italia. Mesi amewashinda Cristiano Ronaldo wa Juventus na Virgil van Dijk wa Liverpool alioingia nao fainali. Kwa upande wa wanawake, Megan Rapince wa Reign FC na timu ya taifa ya Marekani ndiye mchezaji bora akiwashinda Lucy Bronze wa Olympique Lyonnais na Alex Morgan wa Orlando Pride. Tuzo nyingine zilizotolewa usiku huu ni pamoja na ya Kocha Bora kwa timu za wanaume iliyokwenda kwa Mjerumani Jurgen Klop wa Liverpool akiwashinda Pep Guardiola wa Manchester City na Mauricio Pochettino wa Tottenham Hotspur. Jill Ellis aliyekuwa akiinoa Marekani ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Timu za Wanawake akiwabwaga Phil Neville wa Uingereza na Sarina Wiegman wa Uholanzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako