• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya kugharamia matitabu ya wanafunzi waliojeruhiwa baada ya jengo la shule yao kubomoka

    (GMT+08:00) 2019-09-24 10:40:09

    Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus Oguna amesema serikali itagharamia matibabu ya wanafunzi waliojeruhiwa baada ya shule yao kuporomoka katika mji mkuu Nairobi. Wanafunzi 7 walifariki kwenye mksasa huo wa Jumatatu, huku wengine 57 wakijeruhiwa. Wakazi wa eneo hilo wamemtupia lawama mkandarasi aliyejenga shule hiyo yenye zaidi ya wanafunzi 900.

    Mafisa wa zimamoto wa Baraza la jiji la Nairobi na waokoaji kutoka Shirika la Msalaba mwekundu walifika kwenye eneo la tukio kuwaokua watoto waliokwama kwenye kifusi cha jengo hilo na kuwakimbiza majeruhi katika zahanati ya karibu ya St. Joseph na baadaye wale walio na majeraha makubwa walihamishiwa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta.

    Kwa sasa shule hiyo imefungwa huku serikali ikianza uchunguzi kujua chanzo cha jengo hilo kubomoka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako