• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa mambo ya nje wa China ahudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya tabianchi

  (GMT+08:00) 2019-09-24 15:54:16

  Mjumbe maalumu wa rais wa China, ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana amehudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa uliofanyika jana jumatatu mjini New York, Marekani.

  Akihutubia mkutano huo Bw. Wang Yi amesema, China itatekeleza kwa makini mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na makubaliano ya Paris, na kutimiza lengo la mchango wa ndani wa nchi kwa wakati uliopangwa. Ameongeza kuwa China itashikilia kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja" bila uchafuzi, ili kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya kukusanya nguvu zaidi za ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana mabadiliko ya hali ya hewa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako