• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Pikipiki meneo ya mpakani Uganda kusajiliwa

    (GMT+08:00) 2019-09-24 16:54:55
    Mamlaka ya ushuru nchini Uganda URA imeagiza kusajiliwa upya kwa pikipiki zote za Kenya

    Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA) imeamuru usajili upya wa pikipiki za Kenya zinazofanya kazi wilayani Busia na wilaya zingine za mipakani ili kuhakikisha kuwa zinalipa ushuru na kupambana na uhalifu.

    Meneja wa URA katika mkoa wa mashariki mwa Uganda Bwana James Malinzi, amesema mamlaka hiyo inapoteza fedha nyingi kwa sababu Waganda kwenye wilaya za mpakani wanapendelea kununua pikipiki na kukosa kubadilisha usajili.

    Kulingana na maafisa wa URA, wamiliki wa pikipiki wanatakiwa kulipa ada ya kati ya dol $ 200 na $ 400 kulingana na hali ya pikipiki.

    Katik wilaya Busia, kuna jumla ya pikipiki 2,000 za Kenya zilizosajiliwa lakini zilez Uganda ni chini ya 300.

    Waendeshaji pikipiki kwenye eneo hilo wamesema wanapendelea kununua pikipiki kutoka Kenya kwa sababu ni nafuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako