• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Uchukuzi wa anga kuongezeka mara mbili Kenya

    (GMT+08:00) 2019-09-24 16:55:18
    Chama cha kimataifa cha usafiri wa anga IATA kimesema sekta ya uchukuzi wa anga nchini Kenya utakua kwa zaidi ya mara mbili ndani ya miaka 20 ijayo.

    Kulingana na IATA sekta hiyo itakua kwa asilimia 249 na kuiletea Kenya dola bilioni 11.3 kwa mwaka na pia kuwa na nafasi za ajira 859,000 ifikapo 2037.

    Ripoti ya IATA pia inasema sekta hiyoya uchukuzi wa anga iliiletea Kenya dola bilioni 3.2 mwaka 2017 ikiwa ni mchango wa asilimi 4.6 kwenye pato la kitaifa.

    Kenya ilipokea abiria wa nje milioni 4.8 mnamo 2017, ambayo ilisaidia upatikanaji wa kazi 410,000.

    Karibu dola bilioni 0.9 zilitumiwa moja kwa moja na abiria, ambazo ilisaidia kazi 15,000.

    Kulingana na ripoti hiyo ya IATA, Afrika inabaki kuwa chanzo kikubwa cha abiria wanaoingia Kenya, wakiwa ni milioni 3.1 au asilimia 70 ya wageni jumla mwaka 2017. Ulaya inafuata na abiria 585,000 wakifuatiwa na Asia-Pacifiki 284,000, Mashariki ya Kati, 233,000 na Amerika 210,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako