• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukuaji wa uchumi wa China wachangia zaidi katika ongezeko la uchumi duniani

    (GMT+08:00) 2019-09-24 17:05:24

    Mkutano wa kwanza na waandishi wa habari kwa ajili ya kuadhimisha Miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China umefanyika leo mjini Beijing. Naibu mkurugenzi wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China ambaye pia ni mkurugenzi wa Idara ya takwimu ya China Bw. Ning Jizhe amesema kwenye mkutano huo kwamba, ukuaji wa uchumi wa China umechangia zaidi kwa ongezeko la uchumi. Mkurugenzi wa Benki ya Umma ya China Bw. Yi Gang ameeleza kuwa, kadri mambo ya fedha yanavyozidi kuimarishwa, ndivyo utaratibu wa sekta hiyo unaofunguliwa kwa nje ambao una ushindani wenye usawa umethibitishwa kwa kimsingi.

    Katika mkutano huo, Bw. Ning Jizhe ameeleza kuwa, kuanzia mwaka 1952 hadi 2018, wastani wa pato la taifa GDP wa China uliongezeka kutoka yuan 119 hadi elfu 64.6, likiwa ni ongezeko mara 70. Anasema:

    "Hivi sasa China imekuwa nchi kubwa ya pili kwa uchumi duniani, nchi kubwa ya kwanza kwa biashara ya mizigo na akiba ya fedha za kigeni, nchi kubwa ya pili kwa biashara ya utoaji wa huduma, matumizi ya fedha za kigeni na uwekezaji kwa nchi za nje. "

    Bw. Ning Jizhe ameeleza kuwa, katika miaka 70 iliyopita, si kama tu China imepata maendeleo makubwa katika mchakato wa kubadilika kuwa nchi ya viwanda vya kisasa kutoka nchi ya kilimo, bali pia imeonesha umuhimu mkubwa katika ujenzi wa amani ya dunia, kutoa mchango kwa ajili ya mendeleo ya dunia pamoja na ulinzi wa utaratibu wa kimataifa. Akisema:

    "Hivi sasa China ni nchi inayotoa askari wengi zaidi wa kulinda amani kati ya nchi wajumbe wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ukuaji wa uchumi wa China umechangia zaidi kwa ongezeko la uchumi duniani, China siku zote inaunga mkono utaratibu wa pande nyingi, na kufuata kanuni ya biashara huria, na kushiriki katika harakati mbalimbali za mashirika ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa. Pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' lililotolewa na China limeungwa mkono na nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 160 duniani."

    Mkurugenzi wa Benki ya Umma ya China Bw. Yi Gang ameeleza kuwa, katika miaka 40 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, utaratibu wa soko la fedha wenye ushindani umeanzishwa kwa kimsingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako