• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mafanikio ya China yanategemea nguvu bora ya mfumo

  (GMT+08:00) 2019-09-24 19:45:57

  Wakati Jamhuri ya watu wa China inapoadhimisha miaka 70 tangu ianzishwe, uchumi ya China umetimiza maendeleo makubwa. Takwimu zinaonesha kuwa pato la taifa la China GDP la mwaka 2018 limeongezeka mara 174 ikilinganishwa na la mwaka 1952, ambalo linachukua asilimia 16 ya uchumi wa dunia. Thamani ya biashara ya nje imeongezeka kutoka dola bilioni 1.13 za kimarekani za mwaka 1950 na kufikia dola trilioni 4.6 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la mara 4000. Mfumo wa biashara na nje wa China umetimiza ongezeko la kiwango cha juu ambao umeendeleza kutoka kuuza bidhaa za ngazi ya chini ukiwemo mchele, hadi bidhaa zenye thamani ya juu ya ziada ikiwemo reli ya kasi.

  Katika miaka 70 iliyopita, China imekua kutoka nchi yenye hali duni ya kiuchumi na kiwango cha chini cha sayansi na teknolojia, hadi kuwa nchi kubwa zaidi kiviwanda, biashara ya mizigo, na akiba ya sarafu za kigeni duniani. China pia inafanya juhudi kuhimiza mfumo wa pande nyingi, kutoa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na wazo la jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na kutoa mchango mkubwa katika usimamizi wa dunia kwa hatua halisi. Matokeo hayo hayakupatikana kwa bahati, bali yaliyotokana nguvu bora ya mfumo wa China, na China siku zote itashikilia njia inayofaa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako