• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanajeshi elfu 15 kushiriki kwenye Gwaride la Siku ya Taifa la China

  (GMT+08:00) 2019-09-25 08:30:55

  Gwaride kubwa la kijeshi kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya taifa la China litakalofanyika Oktoba Mosi mjini Beijing, litashirikisha wanajeshi wapatao elfu 15.

  Kwa mujibu wa ofisi ya uongozi wa gwaride hilo litakalofanyika katika mtaa wa Chang'an katikati ya mji wa Beijing kwa dakika 80, gwaride hilo litakuwa kubwa zaidi kufanyika katika miaka ya karibuni, ambapo jumla ya vikosi 59 na bendi moja ya kijeshi, ndege zaidi ya 160 na vifaa 580 vya kijeshi vya aina mbalimbali vitashiriki.

  Naibu mkurugenzi wa ofisi ya uongozi wa gwaride hilo Meja Jenerali Cai Zhijun amesema, gwaride hilo ni la kwanza kufanyika tangu China iingie kwenye zama mpya, na lengo lake ni kuonesha dhamira thabiti ya jeshi la China ya kulinda mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya nchi, na pia kulinda amani ya dunia na utulivu wa kikanda. Amesema vifaa na silaha nyingi mpya zitaoneshwa kwa mara ya kwanza kwenye gwaride hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako