• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Kenya kukabiliwa na tishio la marufuku kufuatia madai ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli

  (GMT+08:00) 2019-09-25 09:13:25

  Siku chache kabla ya Riadha za Dunia kuanza Ijumaa ya Septemba 27 jijini Doha nchini Qatar, Kenya inakabiliwa na tishio la kupigwa marufuku na Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) baada ya televisheni moja nchini Ujerumani kufichua uozo zaidi wa matumizi ya dawa za kusisimua misuli miongoni mwa wanariadha wa Kenya. Mkuu wa Kitengo cha Maadili ya Riadha kwenye shirikisho hilo (AIU), Brett Clothier alisema Kenya huenda ikachukuliwa hatua hiyo baada ya kupokea ushahidi kutoka televisheni ya ZDF yenye makao yake mjini Mainz kuwa wanariadha wengi wa Kenya wanatumia dawa aina ya EPO kujiongeza nguvu. Katika ufichuzi wake, televisheni hiyo inadai kuwa wanariadha wawili wa kike na kiume walio katika timu ya Kenya inayojiandaa kuelekea Doha wametibiwa na dawa ya EPO. Afisa mmoja wa Shirikisho la Riadha nchini Kenya (AK) Barnabas Korir, alizungumzia ufichuzi huo akisema wanahakikisha kuwa timu yao ya taifa inafuata sheria na walizungumza sana na timu na kuiandalia warsha ya kueleza sheria zote za kimataifa na pia kupima wanariadha mara kadhaa. Mwaka 2015 na 2016, Kenya iliponea chupuchupu kukosa michezo ya Olimpiki na mashindano mengine kutokana na uovu huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako