• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ataka hatua zaidi zifuatwe ili kutimiza SDGs

    (GMT+08:00) 2019-09-25 09:41:53

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana ametoa wito kwa nchi zote duniani kuchukua hatua zaidi kwa ajili ya kutimiza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) ifikapo mwaka 2030.

    Katika taarifa iliyotolewa kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa maendeleo endelevu, Bw. Guterres amesema, ahadi za ajenda ya mwaka 2030 ni za wazi, lakini bado hazijatekelezwa kikamilifu kama inavyotakiwa.

    Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi amesema, ajenda ya mwaka 2030 imefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa maendeleo wa dunia nzima. Amesema inapaswa kuzingatia ufuatiliaji wa nchi zinazoendelea, kuhimiza maendeleo yanayoendana na uchumi, mazingira na jamii, na kuchukua hatua zenye ufanisi kuzidisha uhusiano wa kiwenzi wa maendeleo ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako