• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwanja mpya wa ndege wa Daxing utakuwa injini mpya ya maendeleo ya China katika kuhimiza mawasiliano na dunia

    (GMT+08:00) 2019-09-25 18:08:40

    "Natangaza, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Daxing wa Beijing umezinduliwa rasmi." Ni sauti yake rais Xi Jinping wa China akitangaza kuzinduliwa rasmi kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Daxing alipohudhuria hafla ya uzinduzi wa uwanja huo wa ndege iliyofanyika sehemu ya Daxing hapa Beijing. Katika siku za baadaye, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Daxing wa Beijing utakuwa alama mpya ya ujenzi na uendeshaji wa kituo cha safari za anga cha kimataifa na injini mpya ya kuhimiza maendeleo ya pamoja ya sehemu ya Beijing, Tianjing na Hebei. Uwanja huo unawekezwa dola bilioni 63.2 za kimarekani, na safari za ndege zinaenea sehemu 112 duniani. Inakadiriwa kuwa, idadi ya abiria kwa mwaka itafikia milioni 100 na ndege laki 8 zitaruka na kutua katika uwanja huo.

    Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Daxing ambao ni mlango mpya wa nchi wenye kiwango cha juu duniani, umesifiwa na watu kutokana na kuwa umejumuishwa mawazo mapya ya maendeleo ya China ambayo yameonesha uvumbuzi, kutokuwa na uchafuzi na ufunguaji mlango. Gazeti la Uingereza The Guardian limeuweka kwenye nafasi ya kwanza kati ya miujiza mipya saba duniani, na shirika la habari la Marekani CNN pia limeusifu kama ni jengo linalowafurahisha watu zaidi duniani mwaka 2019.

    Uvumbuzi ni moja kati ya alama muhimu za China kwa hivi leo, vilevile ni kiini cha ujenzi wa uwanja huo wa kimataifa ambao umeweka rekodi mpya zaidi ya 40 za China na za kimataifa, pamoja na uvumbuzi wa zaidi ya aina 100 za teknolojia.

    Uwanja huo vilevile umesifiwa kama ni "mlango mpya wa taifa usio na uchafuzi wa mazingira". Na matumizi yake ya nishati yamepungua kwa asilimia 20 kuliko viwanja vingine vya ndege vyenye kiwango kama hicho duniani. Utoaji wake wa hewa za kaboni dioxide utapungua kwa asilimia tani elfu 22 kila mwaka, ambayo ni sawa na kupanda miti milioni 1.19, na kubana matumizi ya tani 8850 za makaa ya mawe.

    Mbali na hayo, hali inayofuatiliwa na watu ni matumizi ya akili bandia na utoaji wa huduma zinazowarahisisha watu kwenye uwanja huo, hali ambayo imeonesha kuwa mradi huo mkubwa umeonesha wazo la kuwahudumia vizuri watu, na pia ni sehemu muhimu kwa China katika kutekeleza kwa kina mageuzi na kuhimiza maendeleo yenye sifa bora.

    Baada ya kuanza kazi kwa uwanja huo, kadiri safari nyingi zaidi za kimataifa zitakazoanzishwa, mawasiliano kati ya nchi zinazojiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" yatakuwa mazuri na ya karibu zaidi, ili kupata ustawi na maendeleo kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako