• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni ya China yasaini makubaliano na chuo kikuu cha Kenya kuboresha mawasiliano ya kifasihi

  (GMT+08:00) 2019-09-26 08:12:52

  Kampeni ya fasihi ya China "China Shelf" imewasili Afrika jumatano, ambapo ujumbe wa China katika Tamasha la Kimataifa la Vitabu la Nairobi ulifanya hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano na upande wa Kenya, huku mamia ya vitabu vinavyoeleza mafanikio ya China vikionyeshwa.

  Kaimu mkuu wa Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya Isaac Mbeche ameeleza kufurahia na kuunga mkono hatua hiyo, na kusema anatarajia kuwa na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Chuo kikuu hicho na chuo cha Confucius na kampuni ya uchapishaji vitabu ya Zhongtu Changjiang.

  Kampuni hiyo imetoa msaada wa vitabu vya watoto kwa Maktaba ya Taifa ya Kenya ili kuanzisha Eneo la Vitabu vya Kichina kwenye maktaba hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako