• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu laki 1 kushiriki maonyesho ya umma katika Siku ya Taifa la China

  (GMT+08:00) 2019-09-26 08:13:33

  Raia laki moja wa China wataandamana katika gwaride la maadhimisho ya Siku ya Taifa la China itakayoangukia Oktoba Mosi.

  Mkurugenzi wa idara ya kuandaa gwaride hilo Zhang Ge amesema, gwaride hilo litajumuisha maboya makubwa 70 yakiwa kwenye makundi 36, na yatapita kwenye Mtaa wa Chang'an mjini Beijing kutoka mashariki kuelekea magharibi. Ameeleza kuwa gwaride hilo litaonyesha mchakato wa kihistoria tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, utekelezaji wa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, na maendeleo ya ujamaa wenye umaalum wa kichina, pia jinsi aina hiyo ya ujamaa ilivyoingia kwenye zama mpya.

  Huu ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako