• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UEFA: Shirikisho la soka Ulaya laongeza mashindano mengine makubwa

  (GMT+08:00) 2019-09-26 09:59:27

  Shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA limetangaza rasmi mashindano mengine mapya ambayo yatafanya kuwa na jumla ya michuano mitatu baada ya miwili iliyokuwa nayo kwa sasa ambayo ni UEFA Champions League na Europa League. Katika kikao chake kilichofanyika nchini Slovenia shirikisho hilo limeazimia kuanzisha michuano hiyo mipya itakayo julikana kama UEFA Europa Conference League ambapo imepangwa kuanza kutimua vumbi msimu wa 2021. Michuano hii imeanzishwa kwa lengo la kuzipa nafasi klabu zinazotoka nchi wanachama wa UEFA ambazo hazipo kwenye viwango vya juu kuweza kupata nafasi zaidi ya kushiriki michuano ya Ulaya. Michuano hii itakuwa ikichezwa siku ya alhamisi kama kawaida na itakuja na mabadiliko kidogo ambapo itapunguza klabu zinazoshiriki michuano ya Europa League ambazo kwasasa ni klabu 64 lakini zitapungua mpaka kufikia klabu 32. Hivyo ligi zote tatu zitakuwa na timu 32 huku zikitengeneza makundi manane na kila kundi likiwa na timu 4.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako