• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Tamaduni na mchenga zatinga fainali ya Sprite Basketball Kings 2019

    (GMT+08:00) 2019-09-26 10:00:46

    Nusu fainali ya Sprite Basketball Kings 2019 imekamilika usiku wa jana katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay ambapo nusu fainali za pili kati ya 'Best of three' zimepigwa. Katika mchezo wa kwanza, Tamaduni imeibuka na ushindi wa vikapu 116 dhidi ya 65 vya KG Dallas huku mchezaji, Cornel Joseph wa Tamaduni akifunga pointi 28, rebounds 10 na assist 1. Katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali wikiendi iliyopita, Tamaduni iliibuka na ushindi wa vikapu 99 dhidi ya 78 vya KG Dallas. Mchezo wa pili wa jana, Mchenga Basketball Stars imeibuka na ushindi wa vikapu 105 dhidi ya 72 vya Flying Dribblers huku mchezaji, Baraka Sadick wa Mchenga akifunga jumla ya pointi 49, rebounds 2 na assist 2. Katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali wikiendi iliyopita, Mchenga Basketball Stars iliibuka na ushindi wa vikapu 95 dhidi ya 71 vya Flying Dribblers. Kwa ushindi huo wa jana, ni rasmi sasa kuwa fainali ya Sprite Basketball Kings 2019 itakuwa kati ya Tamaduni na Mchenga Basketball Stars baada ya kufanikiwa kushinda nusu fainali mbili kati ya tatu dhidi ya wapinzani wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako