• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa "China Shelf" wazinduliwa kwa mara ya kwanza barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-09-26 17:26:27

    Maonesho ya 22 ya Kimataifa ya Vitabu ya Kenya yamefunguliwa jana. Siku hiyo ujumbe wa uchapishaji wa China uliandaa sherehe ya utiaji wa saini wa ushirikiano kuhusu mradi wa "China Shelf" na Kenya, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mradi huo kuzinduliwa barani Afrika.

    Mradi huo unahusisha vitabu vya aina zaidi ya 500, na asilimia 90 kati ya vitabu hivyo imetafsiriwa kwa lugha ya kiingereza, ambavyo vinafaa kwa wasomi wa Kenya haswa vijana na watoto. Mbali na hayo, pia kuna vitabu vya toleo la kichina na lugha ya kiswahili. Meneja mkuu wa Kampuni ya maendeleo ya utamaduni ya Yingjueyi ya Chombo cha habari cha Changjiang Bw. Yang Yunpeng anasema:

    "Mwaka huu tumeweka vituo viwili kwa mradi huo zikiwemo Maktaba ya Taifa ya Kenya na Chuo Kikuu cha Nariobi. Baadhi ya vitabu vitatolewa kama zawadi kwa wenyeji wa huko, vingine vitauzwa madukani"

    Naibu meneja mkuu wa kundi la kundi la vyombo vya habari vya uchapishaji la Changjiang la Hubei Bihua amesema, mawasiliano ya utamaduni ni sehemu muhimu katika mawasiliano kati ya China na Afrika, na China na Kenya. Anasema:

    "Katika mchakato huo wa ushirikiano, tumefurahia kuona kuwa vitabu yenye maudhui ya Kenya vimepokelewa vizuri na wasomaji wa China. Vilevile wananchi wa Kenya pia wanatumai kuzidi kuifahamu China, na kuna mustakabali wa mawasiliano ya utamaduni kati ya pande zetu mbili."

    Kaimu mkuu wa Chuo Kikuu cha Nairobi Bw. Isaac Mbeche amepongeza kampuni ya uchapishaji ya Changjiang kuingia barani Afrika haswa nchini Kenya. Akieleza matumaini yake kuwa bidhaa nyingi zaidi za makampuni ya uchapishaji zitaonekana barani Afrika,ili kuwawezesha watu wa China na Afrika kufahamiana vizuri zaidi. Anasema:

    "Ushirikiano huo kati ya Mradi wa 'China Shelf' na Chuo cha Confucius kwenye Chuo Kikuu cha Nairobi, utatoa fursa nyingi zaidi kwa wanafunzi wetu kusoma vitabu."

    Balozi mdogo wa Ubalozi wa China nchini Kenya Bw. Wang Xuezheng amesisitiza kuwa, ushirikiano huo utazidi kusukuma mbele mawasiliano ya utamaduni kati ya watu wa China na Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako