• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani na Japan zasaini makubaliano ya awali ya biashara

    (GMT+08:00) 2019-09-26 18:37:21

    Rais Donald Trump wa Marekani na waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe wamesaini makubaliano ya awali ya biashara, ambayo yatafuta au kupunguza ushuru wa forodha kwa bidhaa za kilimo na viwanda isipokuwa magari.

    Kwenye hafla ya kusaini makubaliano hayo rais Trump amesema makubaliano hayo ni hatua muhimu kwa Marekani na Japan kufikia makubaliano ya biashara ya kunufaishana na yenye usawa. Japan itafungua soko lake kwa bidhaa za Marekani zenye thamani ya dola bilioni 7 za kimarekani, na kupunguza au kufuta ushuru wa baadhi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani.

    Bw. Shinzo Abe amesema baada ya makubaliano hayo kuanza kutekelezwa, uwekezaji wa Japan nchini Marekani utaongezeka na uchumi wa nchi mbili utakua zaidi, hatua ambayo ni ya kunufaisha pande zote mbili.

    Mjumbe wa mazungumzo ya biashara wa Marekani Bw. Robert Lighthizer amesema nchi mbili zitajadili suala la ushuru wa magari kwenye mazungumzo yatakayofuata.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako