• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China apongeza maadhimisho ya miaka 60 tangu shamba la mafuta la Daqing ligunduliwe

  (GMT+08:00) 2019-09-26 18:41:26

  Rais Xi Jinping wa China ametoa barua ya pongezi na salamu za pongezi kwa viongozi, wafanyakazi, na wastaafu wa shamba la mafuta ya petrol la Daqing lililoko mkoani Heilongjiang, baada ya shamba hilo kutimiza miaka 60.

  Rais Xi amesema katika miaka hiyo 60 iliyopita, kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China CPC ilifanya uamuzi mkubwa wa uhamiaji wa kimkakati wa utafutaji wa mafuta kwa upande wa mashariki, wafanyakazi wengi walifanya juhudi kugundua shamba hilo na kujenga kituo kikubwa zaidi cha uzalishaji wa mafuta. Mchango mkubwa unaotolewa na shamba hilo na moyo wa wafanyakazi wa shamba hilo, umekuwa sehemu muhimu ya moyo mtukufu wa wachina.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako