• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Utafiti unaonyesha kuwa Afrika ni eneo la pili kwa ukuaji wa Utalii duniani

  (GMT+08:00) 2019-09-26 19:56:30

  Kusafiri na utalii ni mojawapo wa vichocheo vikubwa vya uchumi wa Afrika,na kuchangia asilimia 8.5 ya pato la taifa kwa mwaka 2018, sawa na $194.2 bilioni.

  Kulingana na Ripoti ya Jumia ya Ukarimu Afrika,ukuaji huu umeiweka Afrika kama eneo la pili linalokua kwa kasi kwa utalii duniani,likiwa na ukuaji wa asilimia 5.6 baada ya Asia Pacific na dhidi ya wastani wa ukuaji wa asilimia 3.9 duniani.

  Afrika ilipokea watalii wa kimataifa milioni 67 mwaka 2018,na kuandikisha ongezeko la asilimia 7 kutoka watalii milioni 63 mwaka 2017 na milioni 58 mwaka 2016.

  Ongezeko hili la taratibu linatokana na uwezo na unafuu wa kusafiri haswa barani Afrika,huku watalii wa ndani wakiandikisha jumla ya asilimia 56 ya matumizi yote ikilinganishwa na matumizi ya watalii wa kimataifa ya asilimia 44.

  Pamoja na hayo,safari za burudani bado ni sehemu muhimu ya sekta ya utalii barani Afrika,ikichukua asilimia 71 ya matumizi ya watalii mwaka 2018.

  Mkuu wa Usafiri katika Shirika la Jumia,Estelle Verdier,alisema kuwa utekelezaji wa eneo huru la biashara Afrika (ACFTA) unatarajiwa kuongeza uafiri wa ndani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako