• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa waraka mweupe kuhusu China na dunia katika zama mpya

  (GMT+08:00) 2019-09-27 12:14:53

  Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China imetoa waraka mweupe wenye kichwa cha habari "China na Dunia katika Zama Mpya".

  Licha ya utangulizi na hitimisho, waraka huo unajumuisha sehemu nne: "China Imepata Njia ya Maendeleo Inayoendana na Hali Yake Halisi", "Maendeleo ya China ni Fursa kwa Dunia", "Dunia Nzuri na Yenye Ustawi ni Nia ya Watu Wote", na "China Inachangia Katika Kujenga Dunia Bora".

  Waraka huo umesema, China imeingia katika zama mpya ya maendeleo, na sasa ina athari kubwa katika dunia ambayo ni ya kina zaidi, halisi, na ya muda mrefu, na kwamba dunia kwa sasa inaifuatilia kwa makini China.

  Huu ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Katika miaka 70 iliyopita, chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, nchi hiyo imeshuhudia mabadiliko makubwa na kutimiza maajabu ya maendeleo ambayo hayajatokea katika historia ya binadamu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako