• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi za EAC zatakiwa kushusha gharama za uzalishaji

  (GMT+08:00) 2019-09-27 18:38:33

  Licha ya mafanikio ambayo yamepatikana tangu kuanzishwa kwa Itifaki ya Ushuru wa Forodha, nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimeaswa kushusha gharama za uzalishaji bidhaa ili kuchochea kupunguza kiwango kikubwa kutokua soko la bidhaa kutoka mataifa makubwa.

  Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kanda wa Kenya, Adan Mohamed amesema hayo leo wakati wa mkutano wa sekta ya biashara ambao ni sehemu ya miaka 20 tangu kuanzishwa EAC.

  Amesema kumekua na mafanikio ya kujivunia lakini bado nchi wanachama zinaweza kufanya zaidi ili kuwafanya wananchi wa nchi sita zinaunda EAC kufurahia mtangamano huo.

  Awali, Naibu Katibu Mkuu wa EAC, Stephen Mlote amesema yapo mafanikio ya kupigiwa mfano tangu kuanzishwa jumuiya hiyo ambayo yamerahisisha uvukaji mipaka ya nchi wanachama kwaajili ya kufanya kazi, kutoa huduma na kuanzisha biashara katika nchi za EAC.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako