• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China azungumzia masuala makuu ya dunia katika hotuba ya UM

    (GMT+08:00) 2019-09-28 17:34:31

    Mjumbe wa taifa la China ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi Ijumaa alitoa hotuba kwenye mjadala wa kawaida wa kikao cha 74 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika mjini New York, akigusia masuala mbalimbali kutoka maendeleo hadi vitendo vya kujilinda na sera ya upande mmoja, na amani na haki za dunia. 

    Katika hotuba yake, Wang amesema mafanikio ya maendeleo ya China yanatokana na kushikilia uongozi wa pamoja uliodhibitiwa wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC, njia ya maendeleo inayoendana na hali ya taifa la China, sera ya msingi ya taifa ya mageuzi na kufungua mlango, na falsafa ya maendeleo yanayozingatia maslahi ya wananchi.

    Akikumbusha kuwa mwaka 2019 inaadhimishwa miaka 70 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, Wang amesema katika miongo saba iliyopita, wachina wamebadilisha hatma yao kupitia juhudi zisizosita huku China ikijitahidi kujiunga na dunia na kutoa mchango wake kwa ajili ya amani na ustawi wa dunia. Amesema China imeshuhudia safari yenye mitihani na changamoto, lakini bado inashikilia madhumuni ya awali na kwamba China inaongozwa na kanuni ya uhuru, kuamini usawa kati ya nchi tofauti, kulinda haki na kutafuta ushirikiano unaozinufaisha pande zote.

    Ameongeza kuwa utaratibu wa kimataifa unatakiwa kuendana na sheria na kanuni, na vitendo vya kukiuka kanuni za kimataifa vinaweza kuitumbukiza dunia kwenye machafuko. Amesema dunia ya leo sio mahali salama, na sera ya upande mmoja na vitendo vya kujilinda vinatoa vitishio vikubwa kwa uratibu wa kimataifa, kwa hivyo China iko tayari kushirikiana na pande nyingine kutekeleza wajibu wake kama nchi kubwa ili kulinda amani na haki ya dunia.

    Ameeleza kuwa wakati hatma ya dunia inakabiliwa na hatari, China haitaangalia tu na ikiwa mjumbe mwanzilishi wa Umoja wa Mataifa, inafanya kazi na nchi nyingine kujenga aina mpya ya mahusiano ya kimataifa na jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Wang amesema maendeleo ni ufunguo mkuu wa kutatua matatizo yote, na yanatakiwa kuwekwa katikati ya utaratibu wa sera ya jumla ya dunia, ikiwa inazingatia maeneo yanayopewa kipaumbele kama kupunguza umaskini, miundombinu, elimu na afya ya umma.

    Amesema Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja linalenga kutimiza maendeleo yaliyo wazi, kijani na safi na yaliyo ya ngazi ya juu, endelevu na kuangalia maslahi ya wanananchi. Ametoa wito kwa nchi nyingine kutumia vizuri fursa za maendeleo zinazotokana na Pendekezo hilo na kuongeza nguvu mpya ya msukumo kwa ajili ya kutekeleza Ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako