• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwekezaji mkubwa wa China kwenye elimu waandaa watu wenye uwezo wa kuhimiza maendeleo ya ngazi ya juu

    (GMT+08:00) 2019-09-28 20:45:32

    Wakati Jamhuri ya Watu wa China ilipoanzishwa, asilimia 80 ya watu walikuwa hawajapata elimu ya shule. Baada ya miongo saba, China imekuwa na walimu zaidi ya milioni 16, elimu ya lazima ya miaka tisa imefika karibu sehemu zote za nchi. Karibu nusu ya nguvukazi mpya wamepewa elimu ya juu, na wastani wa muda wa masomo umefikia miaka 13,6. Mwaka jana, dola za kimarekani zaidi ya bilioni 645 ziliwekezwa kwenye elimu kote nchini, na elimu imekuwa sekta inayowekezwa zaidi kwenye matumizi ya umma.

    Kwa China yenye watu bilioni 1.4, ni changamoto kubwa ya kifedha kueneza elimu ya lazima. Mwaka 1986, China iliamua kutoa sheria ya elimu ya lazima, na kutimiza lengo hilo baada ya miongo miwili na zaidi. Wakati huohuo, utaratibu wa elimu ya juu na elimu ya ufundi stadi pia umejengwa. Katika miongo saba iliyopita, watu milioni 270 wenye sifa bora wameandaliwa. Kama tunasema katika kipindi cha mwanzo cha utekelezaji wa mageuzi na ufunguaji mlango, China ilitimiza ukuaji wa uchumi kwa kutegemea sekta inayohitaji nguvukazi nyingine, na katika siku za baadaye, China itatimiza maendeleo mazuri ya kiuchumi kwa kupitia maendeleo yenye sifa nzuri na kutegemea sekta yenye thamani kubwa ya nyongeza. Katika mchakato huo, uwekezaji mkubwa wa China kwenye elimu umezidi kuonesha ufanisi wake katika kuandaa watu wenye uwezo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako