• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi awatunukia watu waliopewa nishani za taifa na tuzo za heshima

    (GMT+08:00) 2019-09-29 16:21:17

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekabidhi nishani za taifa na tuzo za heshima za Jamhuri ya Watu wa China kwa watu waliotunukiwa nishani hizo.

    Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na mwenyekiti wa Tume Kuu ya Jeshi aliwasaidia watu hao kuvaa nishani hizo na kushikana mikono nao.

    Akihutubia hafla hiyo rais Xi ametoa pongezi na heshima kwa mashujaa na watu wa mfano wa kuigwa waliotunukiwa nishani ya Jamhuri na tuzo za heshima, na marafiki wa nchi za nje waliotunukiwa Nishani ya Urafiki.

    Akiwataja waliotunukiwa nishani hizo kama ni wawakilishi wakubwa wa watu waliochangia shughuli za Chama na watu, rais Xi amesema vitendo na michango yao itaadhimishwa kwenye historia ya Jamhuri ya Watu wa China. Amesema wakati watu wanapoheshimu na kuwatetea mashujaa wao, mashujaa wengi wataonekana, na kuongeza kuwa Chama na taifa linatilia mkazo katika kuwaheshimu mashujaa na watu wa mfano wa kuigwa ili kueneza sifa zao bora za utiifu, uvumilivu na unyenyekevu. Amesisitiza utiifu wao kwa shughuli za Chama na watu, kujituma kwao kwa kazi kwa miongo kadhaa bila kusita kwenye maeneo ambayo Chama na watu wanawahitaji zaidi, na unyenyekevu wao wa kujitolea sana katika kazi za kawaida bila kutafuta umaarufu na maslahi binafsi.

    Vilevile rais Xi amewashukuru wageni waliotunukiwa Nishani ya Urafiki kutokana na mchango wao kwa maendeleo ya China, na kusema watu wa China wanapenda kushirikiana na watu wa nchi zote, ili kujenga jamii ya binadamu yenye hatma ya pamoja na kuifanya dunia iwe mahali pazu

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako