• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Braima Dabo asifiwa kwa kumsaidia mwenzake aliyekaribia kuzimia

  (GMT+08:00) 2019-09-30 10:21:10

  Mwanariadha kutoka Guinea-Bissau, amewagusa wengi kote ulimwenguni na pia kusifiwa baada ya kumsaidia mshindani wake kumaliza mashindano. Braima Dabo, ambaye alikuwa akishiriki mashindano ya riadha za dunia jijini Doha, mnamo Ijumaa, Septemba 27, alimsaidia Aruban Johnathan Busby ambaye alikuwa anakaribia kuzimia kwa kumsaidia kumaliza mbio za mita 5,000. Licha ya uwanja kuwa na vifaa vya kupunguza joto, inaaminika kuwa Busby alilemewa katika awamu ya mwisho ya mbio za mita 5, 000 wakati Dabo ambaye alikuwa mbele yake alisimama ili kumsaidia. Inaelezwa kuwa Busby alikuwa akikaribia kuzirai, lakini Dabo alilazimika kumburuta huku mwanariadha huyo akionekana kuchechemea hadi nyumbani huku mashindano yakiendelea kunoga ugani Khalifa. Wawili hao walimaliza mbio hizo dakika tano baada washindani wenzao kumaliza mbio hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako