• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Generation Foot ya Senegal yagomea mechi na kuishitiki Zamalek na CAF kwa kubadilisha ratiba ndani ya saa 24

    (GMT+08:00) 2019-09-30 10:21:36

    Imeelezwa kuwa klabu ya Generation Foot ya Senegal imegoma kucheza mchezo wa raundi ya pili katika Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek, sababu ni Zamalek kubadilisha siku ya mchezo na uwanja ndani ya saa 24. Awali mchezo huo ulipaswa ufanyike juzi kwenye uwanja wa PetroSport lakini ulisongezwa mbele hadi jana katika dimba la Borg El Arab uliopo Alexandria. Generation Foot ambayo ilishinda mchezo wa kwanza kwa mabao 2-1 imefunga safari ya kurejea Senegal na kusema itawashitaki Zamalek na CAF kwenye mahakama ya CAS kwa kutofuata taratibu za mpira baada ya kubadili uwanja na siku ya mchezo ndani ya saa 24 tu.

    Katika siku ya pili ya mashindano hayo ya Doha ambayo ni Jumamosi, Septemba 28, Mwanariadha Ruth Chepngetich, aliwapiku washindani wake na kuishindia Kenya nishani ya dhahabu katika mashindano ya Riadha za Dunia ya IAAF yanayoendelea jijini Doha. Bingwa huyo mwenye umri wa miaka 25, alikata utepe kwa muda wa saa 2:32:43, na kuwabwaga wanariadha mahiri wa Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako