• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bekele ainusia rikodi ya dunia ya Kipchoge katika mashindano ya Marathon ya Berlin

    (GMT+08:00) 2019-09-30 10:22:36

    Mkimbiaji wa Ethiopia Kenenisa Bekele safari hii amekuwa bingwa wa Marathon ya Berlin 2019. Bekele amekata utepe baada ya kukimbia kwa saa mbili dakika moja na sekunde 41 ambapo alibakisha sekunde mbili tu kuifikia rikodi ya dunia iliyowekwa na Eliud Kipchoge katika mbio za mwaka jana. Kipchoge, ambaye anashikilia rikodi ya saa mbili dakika moja na sekunde 39, mwaka huu hakushiriki hivyo kutoweza kutetea taji lake. Hata hivyo mkimbiaji huyo anatarajiwa kushiriki mbio za "Ineos 1:59 Challenge" huko Vienna, Austria mnamo October 12 ambako anataka kuandika historia ya kuwa mtu wa kwanza duniani kukimbia marathon chini ya saa mbili. Ilikuwa ni siku njema kwa wanariadha wa Ethiopia waliotawala marathon ya mwaka huu baada ya Wakenya kuondolewa katika hatua za mwanzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako