• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inayojiendeleza kwa amani siku zote inatuliza maendeleo ya dunia

    (GMT+08:00) 2019-09-30 19:32:40

    Serikali ya China hivi karibuni imetoa waraka wenye jina "China na dunia katika zama mpya", na kufafanua kuwa katika miaka 70 iliyopita, wakati China ilipojiendeleza kwa kujitegemea na kufanya kazi kwa bidii, imeleta manufaa makubwa kwa amani na maendeleo ya dunia. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ya "China inayojiendeleza kwa njia ya amani siku zote yatuliza maendeleo ya dunia".

    Mwaka 2009, msomi wa Uingereza Bw. Martin Jacques alitoa kitabu cha "Wakati China inapoendesha dunia", na kuona kuwa kutokana na hali tofauti ya kihistoria na kiutamaduni, China itakuwa na njia tofauti ya kujiendeleza na nchi za magharibi, na hali hii itaibadilisha dunia nzima kwa kina.

    Amani na maendeleo ni matumaini ya pamoja ya binadamu wote. Lakini kwa bahati mbaya, vita na migogoro vimechukua muda mwingi zaidi kwenye historia ya binadamu. Katika zama za karibuni, nchi za magharibi zilijiendeleza kwa kufanya ukoloni na uvamizi, haswa vita kuu mbili za dunia zilileta maumivu makubwa kwa jamii ya binadamu. Katika miaka 30 iliyopita tangu kumalizika kwa vita baridi, nchi za magharibi zimefanya vita mpya katika sehemu mbalimbali, ambao zimesababisha hali ya msukosuko wa kibinadamu, msimamo mkali na ugaidi.

    Ikiwa nchi kubwa inayothamani zaidi amani, katika miaka 70 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, China haikuchochea vita na mgogoro na nchi yoyote, na pia haikushambulia nchi yoyote. Katika miaka 40 iliyopita, China imebadilikana kuwa nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani kutoka nchi maskini. Sababu kuu ni kwamba China imejiendeleza kwa amani.

    China imechangia mawazo na busara yenye thamani kubwa kwa jumuiya ya kimataifa. Kwa mfano China inafuata sera ya kidiplomasia ya amani na kujiamulia, na kutetea kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani, ambazo zimekuwa kanuni za kimsingi ya kimataifa. Katika miaka ya hivi karibuni, China imetoa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na mawazo ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. China pia inashikilia sera ya ulinzi ya kujilinda, na kuifanya bajeti ya ulinzi iwe wazi. Kati ya mwaka 2012 hadi 2017, bajeti ya ulinzi ya China ilichukua asilimia 1.3 tu ya pato la taifa, na ni kiwango cha chini zaidi ikilinganishwa na nchi nyingine wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Wakati huohuo, China ni nchi ya pili inayochangia zaidi operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa. China pia inafanya kazi za kiujenzi katika utatuzi wa masuala magumu ya kimataifa, yakiwemo masuala ya nyuklia ya Korea ya Kaskazini na Iran, suala la Syria na suala la Afghanistan. Kutokana na matishio ya usalama wa mtandao wa Internet na anga ya juu, China imeshiriki kwenye mazungumzo ya pande nyingi, na kutetea kujenga utaratibu wa kimataifa ulio wa haki na wenye usawa.

    Bila kujali itakuwa na nguvu kubwa namna gani, China inayojiendeleza kwa kufuata njia ya amani haitaleta tishio lolote kwa nchi yoyote, bali inaleta fursa, na siku zote inatuliza maendeleo ya dunia na kuwa mjenzi wa amani ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako