Kampuni za kamare, ambazo zinadhibiti zaidi ya asilimia 60 ya sehemu ya soko nchini Kenya, zimesema wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya ushuru mkubwa uliowekwa na serikali ambao umefanya biashara hiyo kuwa haina faida tena.
SportPesa, ambayo hapo awali ilionyesha kwamba ilikuwa inarudi kwenye biashara, sasa inasema imesikitishwa na uamuzi wa wabunge wa Kenya wa kutoza ushuru wa asilimia 20 kwa tuzo zote za kamare.
Kufungwa kwa kampuni za kamare itanyima serikali mapato ya kodi karibu na sifuri na itasimamisha uwekezaji wote katika michezo nchini Kenya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |