• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi akutana na wawakilishi wa timu ya mpira wa wavu ya wanawake ya China

    (GMT+08:00) 2019-09-30 20:13:55

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na wawakilishi wa wachezaji na makocha wa timu ya mpira wa wavu ya wanawake ya China iliyoshinda kombe la dunia la mpira wa wavu kwa mwaka 2019, ambao walihudhuria tafrija ya maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.

    Rais Xi amepongeza ushindi wao na kusema ushindi wao umehamasisha mapenzi ya watu wa China kwa taifa lao na kuongeza imani na hisia za fahari zao. Amesisitiza kuwa kujenga kwa pande zote nchi yenye nguvu ya kisasa ya ujamaa kunahitaji kuongeza nguvu katika sekta mbalimbali, ikiwemo kutimiza lengo la kujenga China kuwa nchi yenye nguvu ya michezo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako