• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hafla ya utoaji tuzo ya Urafiki ya serikali ya China yafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2019-10-01 09:00:53

    Hafla ya kutoa tuzo ya Urafiki ya serikali ya China ya mwaka 2019 imefanyika jana hapa Beijing, ambapo naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He ametoa tuzo kwa wataalamu wa nchi za nje.

    Bw. Liu He amepongeza wataalamu 100 waliotunukiwa tuzo kutoka nchi 31, na kusema tangu China mpya kuanzishwa, na hasa tangu China ilipoanza kufanya mageuzi na kufungua mlango, wataalamu wengi wamechangia mambo ya ujenzi ya kisasa ya China, kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya China, na kujenga urafiki mkubwa na watu wa China. Watu wa China watakumbuka daima.

    Ameongeza kuwa, China itajitahidi kuhimiza ushirikiano wa uwezo wa uvumbuzi, kulinda hakimiliki za ujuzi, na kutekeleza sera za kuvutia watu wenye ujuzi, ili kutoa urahisi kwa watu wa nchi za nje kufanya kazi na kuishi nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako