• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwakilishi wa China aitaka jumuiya ya kimataifa itoe uhakikisho wa usalama kwa mchakato endelevu wa siasa nchini Syria

    (GMT+08:00) 2019-10-01 09:03:09

    Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Wu Haitao jana kwenye mkutano wa Baraza la usalama kuhusu suala la Syria, ameitaka jumuiya ya kimataifa itoe uhakikisho wa usalama kwa mchakato endelevu wa siasa nchini humo.

    Balozi Wu amesema hivi karibuni mchakato wa kisiasa wa Syria umepata mafanikio muhimu, ikiwa ni pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kutangaza uundwaji wa kamati ya katiba Jumatatu iliyopita.

    Alipozungumzia mkutano utakaofanyika tarehe 30 mwezi Oktoba kwa ajili ya kamati ya katiba ya Syria, Balozi Wu amesema mafanikio kama hayo yana maana muhimu kwa mchakato wa siasa nchini humo, na China inakaribisha maendeleo hayo.

    Vilevile ameitaka jumuiya ya kimataifa iendelee na juhudi za pamoja dhidi ya ugaidi kwa msingi wa sheria za kimataifa na maazimio husika ya Baraza la usalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako