• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maadhimisho ya Miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China yafanyike kwa shangwe

    (GMT+08:00) 2019-10-01 10:47:53

    Shughuli za maadhimisho ya miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China zimefanyika kwa shangwe kwenye Uwanja wa Tian An Men wa Beijing. Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya Chama Bw. Xi Jinping, ametoa hotuba akieleza kumbukumbu kubwa kwa wanamapinduzi watangulizi na waliojitolea mhanga kwa ajili ya ustawi na neema ya taifa na wananchi, na pia ametoa shukrani za dhati kwa marafiki wa nchi mbalimbali wanaofuatilia na kuunga mkono maendeleo ya China.

    Gwaride kubwa limefanyika baada ya mkutano huo, hili ni gwaride kubwa zaidi la kwanza kwa jeshi la China baada ya kufanyiwa mageuzi na kuzatitiwa zaidi, ambapo wanajeshi wapatao elfu 15 hivi wameshiriki kwenye gwaride hilo. Na baada ya gwaride, watu wapatao laki moja hivi watafanya maandamano ya kushangilia sikukuu ya taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako