• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Beatrice Chepkoech ashinda dhahabu mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji Doha

    (GMT+08:00) 2019-10-01 10:52:00

    Mwanariadha anayeshika rikodi ya dunia ya mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji Beatrice Chepkoech, amejishindia nishani ya dhahabu katika mashindano ya riadha za dunia yanayoendelea jijini Doha, Qatar. Chepkoech alishinda mbio hizo kwa rekodi ya dunia kwa kukata utepe baada ya kutumia muda wa dakika 8:57.84, na kuwaongoza mabingwa wenzake Hyvin Kiyeng na Celliphine Chespol kwa ushindi. Mkenya huyo alifuzu kushiriki fainali za mbio hizo baada ya kuingia kwenye ushindani mkali siku ya Ijumaa, Septemba 27. Kiyeng, ambaye aliibuka mshindi wa mbio hizo mwaka 2015 jijini Beijing aliongoza mbio hizo kufuzu, huku mshindi wa riadha za dunia za wanariadha wasiozidi umri wa miaka 20, Chespol akimaliza wa tatu kwa muda wa dakika 9:24.22.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako