• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kujiendeleza kwa amani ni ahadi thabiti ya China kwa dunia

    (GMT+08:00) 2019-10-01 17:01:04

    Maadhimisho makubwa ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China yamefanyika leo kwenye Uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing. Rais Xi Jinping amehutubia maadhimisho hayo akisema, China itaendelea kushirikiana na nchi nyingine duniani kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Shirika kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri yenye kichwa cha "Kujiendeleza kwa amani ni ahadi thabiti ya China kwa dunia nzima"

    Tarehe Mosi Oktoba mwaka 1949, Jamhuri ya Watu wa China iliasisiwa rasmi. Kuanzia siku hiyo, China yenye utamaduni mkubwa na historia ndefu, ambayo wakati huo idadi yake ya watu ilichukua robo ya watu wote duniani, ilisimama baada ya kuteswa na wavamizi kwa zaidi ya karne moja. Katika miongo saba iliyopita, wananchi wa China wameshikamana na kufanya kazi kwa bidii, na kupata maendeleo makubwa yanayoshangaza dunia nzima, na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya amani na maendeleo ya binadamu.

    Wakati dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita, China inajitahidi bila ya kusita kutimiza lengo lake kuu la kustawisha taifa. Kwenye hotuba yake, Rais Xi amesisitiza kuwa China itashikilia mambo matano muhimu katika mchakato wake wa kujiendeleza.

    Kwanza, China itashikilia uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, hadhi kuu ya wananchi na ujamaa wenye umaalumu wa China. Mambo hayo matatu ni uzoefu mkubwa zaidi wa kujiendeleza wa China katika miongo saba iliyopita, na pia ni tegemeo la kimsingi la China kupata mafainkio mapya katika siku zijazo.

    Pili, kushikilia sera ya "Umoja kwa njia ya amani, na nchi moja, mifumo miwili" ni mawazo ya uvumbuzi na njia mwafaka zaidi ya kutimiza umoja wa taifa, na imetekelezwa katika Hong Kong na Macao kwa mafanikio. Katika siku za baadaye, China itajitahidi kuhimiza maendeleo ya uhusiano wa amani kati ya China bara na Taiwan, na mwelekeo wa kihistoria wa umoja wa taifa hautazuiliwa na mtu yeyote na nguvu yoyote.

    Tatu, kushikilia kujiendeleza kwa amani ni ahadi thabiti ya Chama cha Kikomunisti cha China na watu wa China kwa dunia nzima. Kutokana na kuwa na utamaduni mkubwa, ufahamu wa kina kwa masharti ya kutimiza malengo ya maendeleo, na mwamko kuhusu mwelekeo wa hali ya dunia, China siku zote inasisitiza umuhimu wa kujiendeleza kwa amani. Hii sio kauli tupu ya kidiplomasia na mpango wa muda mfupi, bali ni chaguo thabiti la kimkakati na ahadi nzito.

    China mpya imepitia miongo saba, na imeanza safari mpya. Mshikamano ni chanzo cha nguvu ya China katika kujiendeleza kwa kushikilia mambo matano muhimu. Katika miaka 70 iliyopita, wananchi wa China wameshikamana na kushirikiana bega kwa bega, na kushinda changamoto moja baada ya nyingine. Kwenye tafrija ya kuadhimisha sikukuu ya taifa, rais Xi amechukulia mshikamano kama ni uhakikisho wa mafanikio ya China, hii si kama tu ni majumuisho ya kihistoria, bali pia ni mwelekezo kwa kazi za siku zijazo.

    Wananchi wa China wanaamini kuwa, wakiinua bendera ya mshikamano, na kushikilia mambo matano muhimu, watashinda nguvu yoyote inayotaka kutikisa hadhi ya China na kuzuia maendeleo ya China. China inayofuata kanuni ya kujiendeleza kwa amani na kutafuta mafaikio ya pamoja itatoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani na maendeleo ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako