• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa nchi mbalimbali wapongeza miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China

    (GMT+08:00) 2019-10-01 21:33:28

    Viongozi wa nchi mbalimbali na wakurugenzi wa mashirika ya kimataifa wamemtumia simu au barua Rais Xi Jinping wa China kwa kupongeza miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China.

    Rais Vladimir Putin wa Russia amesema katika maadhimisho ya miaka hiyo ya 70, mimi naipongeza China kwa furaha kubwa zaidi. Katika miaka 70 iliyopita, China imepata mafanikio makubwa kwenye sekta za uchumi, jamii, teknolojia na nyinginezo, pia inafanya kazi muhimu katika kutatua masuala makubwa ya dunia nzima.

    Rais Donald Trump anawatakia wananchi wa China wanufaike na amani na ustawi.

    Kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong-un amesema katika miaka 70 iliyopita, nguvu ya jumla ya China na nafasi yake duniani zimeongezeka sama, historia inaonyesha kuwa ujamaa ni chaguo sahihi na la lazima la watu wa China, na uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China ni uhakikisho wa kimsingi kwa Wachina wapate mafanikio.

    Malkia Elizabeth II wa Uingereza anawatakia watu wa China maisha bora na usalama.

    Rais Ram Nath Kovind wa India amesema India na China zikiwa ni nchi kubwa zinazoendelea zinafanya kazi muhimu katika utaratibu wa kisiasa na kiuchumi duniani, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umepata uhai mpya.

    Rais Frank-Walter Steinmeier wa Ujerumani amesema Ujerumani inapenda kulinda na kupanua uhusiano wa kiwenzi na China.

    Rais Matamela Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema katika miaka 70 iliyopita, China imepata mafanikio makubwa na kuwa nchi inayoongoza kwenye sekta mbalimbali , inasifiwa na nchi nyingi hasa nchi zinazoendelea duniani.

    Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amesema, nchi yake imetiwa moyo na maendeleo makubwa ya China yasiyo ya kawaida katika miaka 70 iliyopita.

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema Kenya inasifu sana jitihada za China katika kulinda amani na usalama wa dunia, kuanzisha utaratibu wa kimataifa chini ya msingi wa kanuni, na kupendekeza kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterress amesema katika miaka 70 iliyopita, China imewafanya watu milioni 850 waondokane na umaskini, ambayo ni mafanikio makubwa kabisa kwenye kazi ya upunguzaji wa umaskini. China imekuwa nguzo kuu kwenye ushirikiano wa kimataifa na utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi. Anatakia China mafanikio makubwa zaidi.

    Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amesema wakati huu muhimu wa kihistoria una maana kubwa kwa China, pia unaonesha urafiki na mshikamano kati ya watu wa Afrika na watu wa China. Uhusiano kati ya Afrika na China umekuwa mfano mzuri unaostahili kusifiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako