• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kocha Alberto Salazar afungiwa Qatar kwa dawa za kusisimua misuli

  (GMT+08:00) 2019-10-02 09:05:42

  Michuano ya ubingwa wa riadha duniani imekumbwa na kashfa ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli baada ya kocha Alberto Salazar kufungiwa kwa matumizi ya dawa hizo, hilo likiwa pigo jipya kwa taswira ya mashindano hayo. Salazar, ambaye anajulikana zaidi kwa kuwa mwalimu wa Mo Farah, Mwingereza ambaye ametwaa ubingwa wa Olimpiki mara nne, amefungiwa miaka minne na Shirika la Kupambana na dawa za Kuongeza Nguvu la Marekani (USada) kwa kukiuka sheria za matumizi ya dawa hizo. Mmarekani huyo mzaliwa wa Cuba na mwenye umri wa miaka 61 amefungiwa baada ya uchunguzi wa takriban mwaka mmoja. Jeffrey Brown, mtaalamu kutoka jimbo la Texas ambaye aliwatibu wanariadha wengi wa Salazar katika mradi unaofadhiliwa na kampuni ya Nike wa Oregon, pia amefungiwa kwa miaka minne. Salazar, ambaye alikana tuhuma dhidi yake, amezuiwa kuingia katika uwanja wowote ambao michuano ya ubingwa wa dunia wa riadha inafanyika baada ya leseni zake kufutwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako