• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ronaldo afunguka kustaafu soka mwakani ama baada ya miaka miwili ili kuendeleza biashara yake

    (GMT+08:00) 2019-10-02 09:07:03

    Cristiano Ronaldo amefunguka kuwa huenda akastaafu mwaka ujao ama miaka miwili ijayo ili kuendeleza biashara yake. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34, amekuwa akishinda tuzo zote za kushindaniwa katika taaluma yake na vilabu vya Sporting Lisbon, Manchester United, Real Madrid na Juventus. Rekodi ya Ronaldo haijawahi kushushwa licha ya umri wake akisalia kwenye mashindano huku akikabiliana na upinzani mkali kutoka kwa Lionel Messi. Bingwa huyo mara tano wa Ballon d'Or, bado ana mkataba na mabingwa wa Italia Juventus ambayo itatamatika msimu wa mwaka 2022 wakati atakapotimu umri wa miaka 37. Ronaldo amekuwa akivuna unono katika biashara zake za mitandaoni ikiwemo kuuza suruali, viatu, manukato, asasi ya kidigitali, hoteli, mikahawa na vyumba vya mazoezi. Mzaliwa huyo wa Ureno alithibitisha kufurahia kupanga maisha yake baada ya soka kwa miaka kadhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako