• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Wizi wa saa wamfukuzisha klabuni Lamine Diaby – Fadiga

  (GMT+08:00) 2019-10-03 10:37:56

  Klabu ya ligi ya daraja la kwanza nchini Ufaransa Nice imemtimua mchezaji wake Lamine Diaby - Fadiga baada ya kukiri kuiba saa yenye thamani ya £62,000 kutoka kwa mchezaji mwenzake Kasper Dolberg. Mshambuliaji wa Denmark Dolberg, 21, aliibiwa saa yake katika chumba cha maandalizi mnamo tarehe 16 mwezi Septemba na kuripoti kwa maafisa wa polisi. Mshambuliaji Fadiga mwenye umri wa miaka 18 ameiwakilisha Ufaransa katika kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18. Kwenye taarifa yake klabu hiyo inasema mbali na maswala ya kifedha na michezo. Klabu ya Nice haiwezi na haitakubali tabia kama hiyo ambayo ni kinyume na lengo la kuwaungunisha wafanya kazi wote wa klabu hiyo na wanachama wote wa Rouge et Noir . Dolberg alijiunga na Nice kutoka klabu ya Ajax msimu huu, huku Diaby - Fadiga akiwa katika klabu hiyo kwa muda wa miaka mitatu. Nice ipo katika nafasi ya sita katika ligi hiyo, na siku ya Jumamosi itacheza ugenini dhidi ya klabu iliyo katika nafasi ya tatu Nantes.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako