• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • VOLIBOLI: Cameroon yaipiku Kenya na kuandaa michuano ya Afrika ya kufuzu Olimpiki ya Tokyo

    (GMT+08:00) 2019-10-03 10:39:27

    Kenya imeshindwa kuipiku Cameroon ila sio kwenye uwanja wa mpira wa wavu bali kwenye kinyangányiro cha kuandaa michuano ya Afrika ya kufuzu Olimpiki inayopangwa kufanyika January 6-12 mwakani. Mataifa hayo mawili, ambayo sasa yamekuwa mahasimu wakubwa kwenye michezo, yaliwania kuandaa michuano ya Afrika ya kufuzu Olimpiki ya Tokyo mwaka 2020. Malkia Strikers imeishinda Cameroon mara mbili katika miezi miwili iliyopita na kulitambia taifa hilo la Afrika ya kati. Lakini kwa jana jioni ilikuwa Cameroon ndio walioondoka na kicheko baada ya Shirikisho la Mpira wa Wavu la Afrika kuthibitisha kwamba Cameroon ndio watakaoandaa michuano hiyo. Cameroon iliandaa michuano ya kufuzu Olimpiki ya Rio 2016 katika mwaka 2015 na kujipatia tiketi ya dezo katika michezo ya majira ya joto. Hata hivyo nchi hiyo ilishindwa mechi zote huko Rio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako