• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wachina wavutiwa na maonesho ya kiutamaduni katika siku za mapumziko

  (GMT+08:00) 2019-10-03 17:08:23

  Wachina wako kwenye mapumziko ya wiki moja kutokana na sikukuu ya Siku ya Taifa, na wengi wao wamevutiwa na aina mbalimbali za maonesho ya kiutamaduni.

  Maonesho ya mafanikio yaliyopatikana katika miongo saba iliyopita tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China yanafanyika mjini Beijing, na kupongezwa na watu wa hali mbalimbali. Naibu mkuu wa Kamati Kuu ya Maendeleo na Mageuzi ya China, ambaye pia ni Mkuu wa Idara Kuu ya Takwimu ya China Bw. Ning Jizhe amesema,

  "Maonesho hayo yanaonesha zaidi ya picha 1,700 na video 180 za kihistoria, pamoja na vitu halisi zaidi ya 650 vya zamani, ikiwemo gari la kwanza lililotengenezwa na China na trekta iliyotumiwa zamani. Licha ya hayo, kuna sampuli karibu 100 kama vile nyumba ya miaka 50 ya karne iliyopita, shughuli za kukabiliana na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2008 mkoani Sichuan."

  Kwenye Jumba la Kitaifa la Makumbusho la China, maonesho ya michoro maarufu na maonesho ya vitu vya utamaduni vyenye thamani kubwa ya maadhimisho ya miongo saba ya China mpya pia yamewavutia watu wengi, haswa watalii kutoka sehemu nyingine.

  Kwenye Jumba la Maonesho ya Filamu la China, maonesho ya filamu ya maadhimisho ya miongo saba tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China yanafanyika. Zaidi ya filamu 200 na vitu 500 vinavyohifadhiwa katika jumba hilo zimeonesha mchakato wa maendeleo ya shughuli za filamu katika miongo saba iliyopita. Mkuu wa jumba hilo bibi Chen Ling anasema,

  "Tumeandaa maonesho hayo ili kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Madhumuni yetu ni kuonesha historia ya Wachina ya kufanya kazi kwa bidii katika miaka hiyo iliyopita kupitia filamu."

  Kuanzia tarehe 16 mwezi uliopita, maonesho ya kuigiza ya "Fanya kazi kwa bidii, Wachina!" yamefanyika mjini Beijing. Mtazamaji bibi Hu anapenda sana maonesho hayo, akisema,

  "Nimeguswa sana, hata nimetokwa na machozi. Napenda sana mtindo, muziki, jukwaa, nyimbo na vitu vingine vingi katika maonesho hayo, kweli ni usanii mzuri sana."

  Wakati huohuo, licha ya Beijing, maonesho ya kiutamaduni pia yanafanyika katika sehemu nyingine mbalimbali. Kwa mfano kuanzia tarehe Mosi Oktoba, Jumba la Opera la Shanghai limefanya maonesho ya ngoma ya "Dongfanghong", mji wa Guangzhou nao umeandaa Maonesho ya mwezi mmoja ya opera na michezo ya kijadi ikiwemo ngoma, opera ya Kiguangdong, na sarakasi. Mji wa Nanjing umeandaa maonyesho ya opera yatakayoendelea kwa miezi miwili, na mji wa Bayannaoer umefanya maonesho ya kaligrafia. Naibu mkuu wa Jumba la Maonesho ya Utamaduni la Hetao bibi Qi Xiuli anasema,

  "Kupitia maonesho hayo, tunaweza kuhisi mvuto wa utamaduni wetu wa kijadi, na kuonesha matumaini yetu katika zama mpya. Tunatakia taifa letu kila la heri."

  Hivi leo utalii wa kiutamaduni umekuwa injini mpya ya matumizi katika siku za mapumziko za sikukuu ya taifa ya China, na hali hii inaonesha kuwa Wachina wameinua kiwango chao cha mahitaij ya maisha bora.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako