• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa Japan atarajia ziara itakayofanywa na rais wa China nchini humo kufungua ukurasa mpya kati yao

  (GMT+08:00) 2019-10-03 19:27:02

  Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ametoa pongezi kwa miaka 70 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China na kutarajia uhusiano kati ya nchi hizo mbili uwe na mustakabali mzuri zaidi.

  Akizungumza na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, Bw. Shinzo amesema, tangu mwaka 1972, nchi hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia, uhusiano wa pande hizo umepata maendeleo makubwa, maelewano kati ya watu wa nchi hizo mbili yanaendelea kuimarishwa, na ushirikiano wa kiuchumi kati yao pia umeongezeka.

  Bw. Shinzo pia amesema, hivi sasa, ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya nchi hizo mbili unaendelea kuendelezwa, na umesukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati yao. Anatarajia kuwa ziara itakayofanywa mwaka ujao na rais Xi Jinping wa China nchini humo itakuwa mwanzo wa ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako