• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mombasa-Wafanyabiashara walalama feri kukatiza shughuli katika kivuko cha Likoni

  (GMT+08:00) 2019-10-03 19:30:58
  Wafanyabiashara mjini Mombasa wameikashifu hatua ya Shirika la Feri kukatiza usafiri kwa muda huku shughli za uopoaji wa miili ya Bi Mariam Kigenda na mwanawe Amanda Wambua waliotumbukia na gari yao katika kivuko cha Feri cha Likoni jumapili zikiendelea,wakisema kuwa kuwa usitishaji huo wa shughuli za Feri unaathiri biashara zao.

  Wafanya biashara hao wadogo walio na vibanda vya mboga eneo la Likoni na wahudumu wa usafiri wa umma walilalamika wakisema hatua hiyo imesitisha kabisa biashara zao,na kuwafanya kupoteza maelfu ya pesa.

  Aidha walisema serikali ingefaa kufungua kivuko cha Mtongwe huku shughuli za uopoaji miili zikiendelea katika kivuko cha Likoni.

  Kituo cha feri cha Mtongwe kilifungwa Agosti 2019 na kinatazamiwa kurudia shughuli zake Machi 2020.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako