• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-Sekta ya utalii inatoa nafasi za ajira 142,000

    (GMT+08:00) 2019-10-03 19:31:17

    Kuna haja ya juhudi zaidi kuendeleza sekta ya utalii na ukarimu nchini Rwanda ili nchi hiyo iweze kufikia malengo ya kutengeneza ajira 200,000 kila mwaka.

    Serikali ya Rwanda inatarajia kuzalisha ajira milioni 1.5 kufikia mwaka 2024.

    Kulingana na Afisa Mkuu wa Utalii wa Bodi ya Utalii Rwanda, Belise Kariza, sekta ya utalii na ukarimu kwa sasa imetoa nafasi za ajira takriban 142,000.

    Kwa kipindi cha miaka 10,utalii umekuwa ukiongoza kwa kuiingizia Rwanda fedha za kigeni.

    Malengo ya serikali ni kuongeza fedha hizo hadi $800m kufikia mwaka 2024.

    Aidha Belise alisema sekta hiyo inachangia asilimia 10 ya pato la taifa Rwanda.

    Ukuaji katika sekta ya utalii na ukarimu nchini Rwanda unatarajiwa kutoa nafasi za ajira 151,000 kufikia mwaka 2030.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako