• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yataka Marekani kutolitumia kisiasa soko la mafuta

    (GMT+08:00) 2019-10-03 20:25:40

    Waziri wa mafuta wa Iran Bijan Namdar Zanganeh amesema Marekani haipaswi kulitumia soko la mafuta kwa makusudi yake ya kisiasa.

    Bw. Zanganeh amesema sekta ya nishati haitakiwi kuingizwa katika mambo ya siasa ili kuzuia uingiliaji usiokaribishwa na usiosaidia kutoka "utawala hasimu" kama serikali ya Marekani. Amesema kujichukulia maamuzi ya upande mmoja hakusaidii kitu na kuipa shinikizo Iran hakutarudisha utulivu na amani katika kanda hiyo na dunia nzima.

    Ameongeza kuwa kitendo cha Marekani cha kutumia kisiasa shinikizo la nishati kitafanya usalama wa usambazaji wa nishati kuwa hatarini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako