• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Mfaransa Kevin Mayer aliaga taji lake la decathlon kwenye mashindano ya Doha

  (GMT+08:00) 2019-10-04 09:41:09

  Juhudi za Kevin Mayer za kutetea taji lake la decathlon katika mashindano ya riadha ya Doha, zimeishia patupu jana Alhamis baada ya Mfaransa huyo aliyejeruhiwa mguu kujitoa kwenye mashindano ya kuruka kwa upondo.

  Mayer, aliyekuwa anaongoza katika msimamo wa jumla wa michezo hiyo baada ya mchezo wa kurusha kisahani, ilimbidi alikodolee macho taji lake likiteketea hivihvi baada ya kushindwa kujisajili katika mashindano ya kuruka kwa upondo. Bingwa huyo wa mwaka 2017 aliyeashindwa kuruka mara mbili, ameshudiwa akijitupa kwenye godoro na kumwaga machozi baada ya juhudi zake za mara ya pili kushindwa. Mayer alionekana dhahiri akichechemea kwenye ufunguzi wa mashindano ya kuruka viunzi mita 110 kwa wanaume. Hata hivyo alirejea na kujisajili kwenye kurusha kisahani akiongoza baada ya mrusho wake pili wa mita 48.34.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako