• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Wachezaji wanne wa Yanga wavunja ukimya waishitaki klabu yao

  (GMT+08:00) 2019-10-04 09:43:24

  Mwenyekiti wa Chama cha Wanasoka Tanzania (SPUTANZA), Musa Kisoky, amethibitisha kupokea malalamiko ya wachezaji wanne wa Yanga, ambao wanaidai klabu hiyo. Kisoky amesema wachezaji Vicent Andrew, Pato Ngonyani, Haji Mwinyi na Matheo Anthony, wamewasilisha malalamiko yao SPUTANZA wakiomba kusaidiwa kudai stahiki zao. Ameeleza kuwa mpaka sasa hatua ambayo wamechukua ni kumwandikia barua Katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao ambapo nakala ya barua hiyo pia imetumwa kwa klabu ili ijibu madai hayo. Kisoky ameongeza kuwa, kinachoendelea sasa ni Katibu mkuu kulifikisha suala hilo mbele ya Kamati Ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji, kwaajili ya kujadiliwa kwa kuhusisha pande zote mbili, lakini ameweka wazi kilichochelewesha kufanyika hivyo, ni kutokana na Sekretalieti nzima ya Yanga kuwa Mwanza katika siku za hivi karibuni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako