• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • LANGALANGA: Madereva kutoka nchi mbalimbali wajisajili kwenye Mbio za Mountain Gorilla Rally za mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2019-10-04 09:43:46

    Madereva kutoka nchi mbalimbali watashiriki kwenye mbio za magari za Mountain Gorilla Rally za mwaka 2019, mashindano ambayo yanaashiria kumalizika kwa msimu wa Mashindano ya Afrika Rally (ARC). Mbio za mwaka huu za Mountain Gorilla Rally zitaanza leo kwenye uwanja wa Amahoro. Madereva wanaoshiriki ni kutoka Burundi, Uganda, Ubelgiji na wenyeji Rwanda, ambapo bingwa wa mwaka 2016, Mrundi dereva Valery Bukera, na wenzake Fahad Massoud, Yunus Mohamed na Roshanali Mohamed Abbas pia wapo kwenye orodha ya madereva watakaoshiriki. Bingwa mtetezi Giancarlo Davite, ambaye anamwongozaji mpya Jan Demeester badala ya Sylvia Vindevogel anatarajiwa kutetea taji lake akiwa na Mitsubishi Lancer Evo X 10. Washiriki wengine kutoka Rwanda ni pamoja na Jean Claude Gakwaya anayeongozwa na Jean Claude Mugabo akiwa na gari aina ya Subaru Impreza N11, pamoja na bingwa wa mbio hizo wa mwaka 2012 Elefter Mitraros.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako